Azimio la Raia wa Dunia


Pale ambapo sisi sote tunaishi dunia hii na tuko jirani miongoni mwetu kuliko siku za nyuma; 

Hali ya kuwa mifumo ya kijamii inaonyesha dalili za kuharibika au kushindwa kabisa na kuleta athari mbali mbali kwa watu duniani; 

Ambapo imekuwa dhahiri miongoni mwa watu wengi kuwa tunahitaji kutathmini upya 

Makisio yetu ya mitazamo ya dunia na kujitwalia michakato mipya ya kifikra (Einstein) 

Ambapo sisi wabina damu bado hatujafikia kilele cha matarajio yetu kukabiliana na ubora wetu kama viumbe, tunashikilia mategemeo makubwa ya maisha bora, ya amani, maisha endelevu na yenye kukidhi jamii ya ulimwengu. 

Pale ambapo mabadiliko makubwa ya kijamii yana asili yake kwenye lugha bayana ya ufasaha (Azimio la Uhuru, la Magna Carta) na mabadiliko ya kweli yamekuja kutoka vikundi vidogo vya kiraia vyenye mwamko wa kifikra (Mead);

 

Sisi ambao tumesaini tunaazimia… Ni haki yetu ya msingi kujizatiti kwenye kanuni zifuatazo:


kuwa raia wawajibikaji wa dunia pamoja na raia wa haki wa mataifa yetu binafsi; 

kujizatiti ili watu wote waishi kwa amani, uhuru na kukidhi mahitaji yao ya msingi; 

kuitwaa falsafa ya “merikebu ya dunia” ambayo inatambua kuwa hatma yetu ni ya muungano na watu wengine usioepukika; (Fuller) 

kuenzi kanuni ya kuwa watu wote wameumbwa kwa usawa, na wanastahili heshima, kuaminiana, utu bila kujali nafasi zao wala tambo lao; 

kuwajibika na ubora wa maisha kwa kizazi kijacho; 

kuwa mabingwa wa haki za kijamii, mazingira endelevu na maridhiano ya kiroho kwa wote; 

kuchukulia maisha yetu na kazi kwa mtazamo wa kutegemeana, uwajibikaji wa binafsi kwa ajili yetu wenyewe na jamii zetu huku tukitegemeana kutunza maisha endelevu ya “wote;” 

kukosoa hulka za upendeleo wa kidaraja kwenye taasisi mbali mbali, uongozi na mfumo mahala popote inaposhindwa kuhudumia jamii yote kwa ujumla; 

kutengeneza miundombinu na kuunga mkono viongozi wapya kama inavyolazimu kwa ajili ya kutimiza mahitaji ya dunia; 

kuwa na uadilifu kwenye kutenda shughuli zetu zote, tushinikize hilo toka kwa raia wenzetu wa sayari hii amabo tunashirikiana na kutegemeana nao; 

kutoa kipaumbele kwenye hii ari, falsafa hizi na vitendo kulingana na dhana ya kutegemeana na uraia wa sayari hii ili wengine waigize kama ambavyo wangefanya wenyewe; 

 

Ahadi

Hivyo sisi tuliosaini, tunaahidi na kuapa mbele ya umma na miongoni mwetu kusimamia kanuni hizi, kusuluhisha na kuwajibika kama wanawake na wanaume waadilifu wanaoshirikiana uraia wa sayari hii.